Rais Xi akutana na Waziri Mkuu wa Singapore, akitoa wito wa kuboresha ushirikiano kati ya China na Singapore

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 25, 2025

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Singapore Lawrence Wong, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma   la Beijing, China, Juni 24, 2025. (Xinhua/Yue Yuewei)

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Singapore Lawrence Wong, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Juni 24, 2025. (Xinhua/Yue Yuewei)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping alikutana na Waziri Mkuu wa Singapore Lawrence Wong mjini Beijing jana Jumanne ambapo amempongeza kwa awamu yake ya pili ya kushika madaraka, na kusema kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 35 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Singapore.

Rais Xi amesisitiza kuwa pande hizo mbili siku zote zinashikilia maelewano na kuheshimiana, huu ni msingi imara wa maendeleo tulivu na mazuri ya uhusiano wa pande mbili.

Rais Xi amesema, "Ushirikiano kati ya nchi hizo mbili umelingana na mwelekeo wa maendeleo ya kazi muhimu ya China katika vipindi mbalimbali, ukitoa matokeo makubwa kama vile Eneo Maalum la Viwanda la Suzhou, matokeo ambayo ni nguvu kubwa ya kusaidia ujenzi wa mambo ya kisasa ya kila nchi kati yao, na pia kuweka kielelezo kwa ushirikiano kati ya nchi za kanda hii."

Ametoa wito kwa pande zote mbili kuchukua uzoefu na hekima kutoka kwenye mchakato wa maendeleo ya uhusiano wa pande mbili, kurithisha na kuendeleza desturi nzuri, na kuwezesha mti wa urafiki wa China na Singapore kustawi na kuzaa matunda tele.

Rais Xi amesisitiza kuwa, China na Singapore zinapaswa kufuata kithabiti mwelekeo mkuu wa urafiki wa pande mbili, na kuutendea na kuuendeleza uhusiano kati ya China na Singapore kwa mtazamo wa juu wa kimkakati na wa muda mrefu.

Ametoa wito wa kuimarishwa kwa msingi wa kisiasa wa urafiki kati ya China na Singapore, kuunga mkono maslahi ya kimsingi na masuala makuu yanayofuatiliwa na kila mmoja wao, na kuzidisha hali ya kuaminiana kisiasa ili kuwezesha maendeleo ya uhusiano wa pande mbili.

"China siku zote inaamini kuwa amani, maendeleo, ushirikiano na kunufaishana ni mwelekeo usiozuilika katika zama tulizonazo," na dunia haipaswi kuwa na umwamba tena au kubururwa kurudi kwenye sheria ya msitu, Xi amesema.

"China inapenda kufanya kazi na Singapore kusimama kwenye upande wa usahihi wa historia na kusimama kwenye upande wa haki na usawa, na kwa pamoja kutetea dunia ya ncha nyingi yenye usawa na utaratibu na utandawazi wa kiuchumi wenye manufaa na jumuishi kwa wote," Rais Xi ameongeza.

Kwa upande wake Wong amesema, urafiki kati ya Singapore na China ulianzia enzi na dahari na umeendelea mpaka sasa, na pande hizo mbili siku zote zinaheshimiana na kuaminiana, ikihakikisha maendeleo tulivu ya uhusiano wa pande mbili na ushirikiano wa karibu.

Singapore itaendelea kushikilia sera ya kuwepo kwa China moja na kupinga kuifanya "Taiwan ijitenge," Wong amesema.

"Kwa kukabiliwa na msukosuko wa hali ya kimataifa, Singapore inapenda kuimarisha uratibu na ushirikiano na China kwenye majukwaa ya kikanda na ya pande nyingi ili kwa pamoja kushikilia mfumo wa pande nyingi na utaratibu wa kimataifa," Wong ameongeza.

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Singapore Lawrence Wong, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma  la Beijing, Juni 24, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Singapore Lawrence Wong, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Juni 24, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha