Njia mpya za uendeshaji wa droni zaanza kutumika katika Mji wa Wuhan katikati mwa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 17, 2025
Njia mpya za uendeshaji wa droni zaanza kutumika katika Mji wa Wuhan katikati mwa China
Picha ya droni iliyopigwa Juni 16, 2025 ikionyesha droni ya kupeleka vifurushi vya wateja ikiruka mjini Wuhan, Mkoa wa Hubei, katikati mwa China. (Xinhua/Wu Zhizun)

WUHAN - Njia kumi mpya za uendeshaji wa droni zinazounganisha sehemu za Wuchang, Hankou na Hanyang mjini Wuhan, Mkoa wa Hubei katikati mwa China zimeanza kutumika rasmi jana Jumatatu, ambapo huduma hiyo ya anga ya chini inahusisha jukwaa la kusimamia droni kidijitali kwa wakati halisi, vituo viwili vya uongozi kwa teknolojia za kisasa, njia 10 za anga ya chini na sehemu 22 za kutua na kuruka kwa droni (aprons) za kutumia teknolojia ya AI.

Huduma hiyo inasaidia kuhimiza maendeleo ya kazi ya kupeleka vifurushi vya wateja kama vile vyakula vya baharini, maua freshi na dawa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha