Marais wa China na Msumbiji watumiana pongezi juu ya maadhimisho ya miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia

(CRI Online) Juni 25, 2025

Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Msumbiji Daniel Chapo leo Jumatano wametumiana salamu za pongezi kusherehekea maadhimisho ya kutimia miaka 50 tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Kwenye ujumbe wake Rais Xi amesema, katika kipindi chote cha miaka hiyo 50, bila kujali hali ya kimataifa inavyobadilika, China na Msumbiji siku zote zimekuwa zikiaminiana na kuungana mkono, na kwamba urafiki kati ya nchi mbili umezidi kuimarika.

Rais Xi ameeleza imani yake kuwa uhusiano wa pande mbili utazidi kuwa na mustakabali mzuri zaidi katika siku za baadaye ilimradi tu pande hizo mbili zitaendelea kushikilia nia ya awali ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia na kusonga mbele bega kwa bega.

Naye Rais Chapo amesema, Msumbiji itaendelea kushikilia sera ya kuwepo kwa China Moja, huku ikiunga mkono juhudi zote za serikali ya China katika kufikia muungano wa taifa.

Amesema, Msumbiji inaunga mkono mapendekezo makuu ya China, na kwamba inapenda kuimarisha uhusiano wa pande mbili katika msingi wa kuheshimiana na kunufaishana, kupanua ushirikiano wa kivitendo, kulinda kwa pamoja mfumo wa pande nyingi na kuhimiza amani, usalama na ustawi wa dunia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha