

Lugha Nyingine
China yatangaza mpango wa maadhimisho ya miaka 80 tangu kupatikana ushindi kwenye vita dhidi ya uvamizi wa Japan
China imetangaza shughuli za maadhimisho ya miaka 80 tangu kupatikana ushindi kwenye Vita vya Watu wa China Kupambana na Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupambana Dhidi ya Ufashisti.
Akizungumza na wanahabari mjini Beijing jana Jumanne, Naibu Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Hu Heping amesema Rais wa China Xi Jinping atahudhuria na kutoa hotuba katika mkutano utakaofanyika asubuhi ya Septemba 3 kwenye Uwanja wa Tian'anmen mjini Beijing, ambalo litajumuisha gwaride la kijeshi.
Kwa mujibu Hu, mchana wa siku hiyo, hafla itafanyika ambapo Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) atahutubia. Pia ameeleza kuwa, jioni ya siku hiyohiyo, tamasha litafanyika na kuhudhuriwa na viongozi wa Chama na serikali.
Hu amesema, katika maadhimisho ya mwaka huu, medali za kuadhimisha miaka 80 tangu kupatikana ushindi wa vita hivyo vya watu wa China dhidi ya uvamizi wa Japan zitatolewa kwa maveterani wa vita na wanafamilia wa maveterani waliofariki.
Amesema shughuli hizo zina umuhimu mkubwa katika kuheshimu historia, kutoa heshima kwa watu waliojitoa mhanga, na kuendeleza moyo wa uzalendo.
Ukumbi wa Kuutazama Mji wa “Kilele cha Tianjin” wa China wafunguliwa rasmi kwa umma
Kuendeleza urithi wa utamaduni usioshikika wa China - ustadi wa kutengeneza chai ya Taiping Houkui
Njia mpya za uendeshaji wa droni zaanza kutumika katika Mji wa Wuhan katikati mwa China
Shughuli za utalii za siku za lavender zahimiza maendeleo ya uchumi katika Mkoa wa Xinjiang, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma