Mjumbe wa Libya asikitikia ukosefu wa mpango wa Umoja wa Mataifa kwa mchakato wa kisiasa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 25, 2025

Balozi wa Libya katika Umoja wa Mataifa Taher El-Sonni akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu hali ya Libya, katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Juni 24, 2025. (Evan Schneider/Picha ya UN/kupitia Xinhua)

UMOJA WA MATAIFA - Balozi wa Libya katika Umoja wa Mataifa (UN) Taher El-Sonni ameelezea masikitiko yake juu ya ukosefu wa mpango wa Umoja wa Mataifa kwa mchakato wa kisiasa katika nchi yake, ambapo baada ya mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa UN kuhusu suala la Libya, Hanna Tetteh kutoa ripoti kwa Baraza la Usalama, balozi huyo wa Libya amesema hakuna jambo jipya katika ripoti yake ndefu.

"Wakati tunakaribisha juhudi za Madamme Tetteh pamoja na timu yake kutafuta mpango wa utatuzi halisi juu ya hali ya kukwama ya kisiasa ya hivi sasa, hata hivyo, hatuwezi kuficha ukweli kwamba hadi sasa hakuna mpango wa kisiasa na hakuna dira dhahiri ambayo imetolewa kwa Walibya," El-Sonni ameliambia Baraza la Usalama.

Amesema, "Walibya bado wanasubiri hili kutoka kwenu kwa kasi kubwa," na Walibya wamekuwa wakitarajia dira kutoka kwa Tetteh katika mkutano huo wa Baraza la Usalama wa Jumanne.

Tetteh ameliambia baraza hilo kuwa atawasilisha dira ya mchakato wa kisiasa nchini Libya katika mkutano ujao, pengine mwezi Agosti.

Ametambua matarajio ya Walibya ya kutangazwa kwa dira hiyo siku ya Jumanne kutokana na hali wasiwasi ya kisiasa ya hivi sasa, lakini amesema kuna haja ya kupitia "mchakato wa mashauriano."

El-Sonni amesema hiyo itamaanisha karibu mwaka mmoja na nusu wa kutokuwepo kwa mchakato halisi wa kisiasa nchini Libya.

Amesema kuwa mwakilishi maalum wa zamani Abdoulaye Bathily alijiuzulu Aprili 2024 na miezi tisa ilikuwa imeshapita wakati Tetteh alipoingia kuchukua nafasi yake Februari 2025 na sasa mpango huo utawasilishwa Agosti, ambayo haimaanishi hata kuzinduliwa kwa mchakato huo.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  kuhusu suala la Libya Hanna Tetteh akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu hali ya Libya,  katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Juni 24, 2025. (Evan Schneider/Picha ya UN/kupitia Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha