Kenya yafanya kongamano kuhimiza ushirikiano wa kilimo na viwanda kati ya China na Afrika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 25, 2025

Hamadi Boga, makamu mkuu wa Muungano kwa Mageuzi ya Kijani barani Afrika (AGRA), akitoa hotuba kwenye mkutano wa kwanza wa Baraza la Afrika na China juu ya Ushirikiano wa Teknolojia ya Kilimo na Viwanda mjini Nairobi, Kenya, Juni 24, 2025. (Xinhua/Li Yahui)

NAIROBI - Mkutano wa kwanza wa Baraza la Afrika na China juu ya Ushirikiano wa Teknolojia ya Kilimo na Viwanda umefanyika Jumanne katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi ambapo mkutano huo wa siku nzima uliandaliwa na Taasisi ya Muungano kwa Mageuzi ya Kijani Barani Afrika (AGRA) yenye makao yake makuu mjini Nairobi, Kituo cha Sayansi ya Kilimo na Uvumbuzi wa Teknolojia cha Beijing Jingwa, Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo na Kituo cha Mambo ya Fedha kwa Ushirikiano wa Kusini-Kusini.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Ibrahim Mayaki, mjumbe maalum wa Umoja wa Afrika kwa mifumo ya chakula, amesema bara hilo liko tayari kupata faida kwa kuiga mfano wa China wa mageuzi ya kilimo, ikichochewa na sera za kutazama mbele, teknolojia na uvumbuzi.

"Tunaweza kutumia maarifa ya mafanikio ya China katika kukifanya kilimo kuwa cha kisasa, mageuzi ya vijijini na kupunguza umaskini kama pointi rejelea za ustawi wa kilimo barani Afrika, wakati huohuo kutambua umaalum wa mifumo ya ikolojia na tamaduni za Afrika," Mayaki amesema.

Hamadi Boga, makamu mkuu wa AGRA, akizungumza kwenye mkutano huo amesema kuwa China imekwenda mbele katika mambo ya kisasa ya kilimo yanayoongozwa na teknolojia na uvumbuzi, ikihamasisha nchi za Afrika kuiga mfano huo, kulisha idadi ya watu inayoongezeka na kupata maendeleo ya kasi katika zama ya viwanda.

Kwa mujibu wa Boga, ushirikiano wa kilimo kati ya China na Afrika, umeendelezwa kwa kasi kama inavyoshuhudiwa kwa uwepo wa uhamishaji teknolojia, uanzishwaji wa maeneo ya kielelezo, ziara za mabadilishano na ushirikiano wa kitaasisi, kuongeza mavuno ya mazao, usindikaji mazao ya kilimo na mauzo ya nje.

Naye Balozi wa China nchini Kenya Guo Haiyan amesema China inapenda kutoa mchango na washirika wa Afrika kuhusu teknolojia yake iliyobuniwa na kuendelezwa nchini mwake, uvumbuzi, uzoefu na mbinu bora, ambazo zinaweza kuharakisha mambo ya kisasa ya kilimo ya bara hilo ili kufikia usalama wa chakula na kuongeza uwezo wa kiushindani wa mauzo ya nje.

Guo amesema kuwa ushirikiano wa kilimo kati ya China na Afrika umeweka kipaumbele kwenye uhamishaji teknolojia, ikiwezesha biashara katika mazao ya kilimo na kuboresha minyororo ya thamani ya mazao ya kilimo.

Mkutano wa kwanza wa Baraza la Afrika na China juu ya Ushirikiano wa Teknolojia ya Kilimo na Viwanda ukifanyika mjini Nairobi, Kenya, Juni 24, 2025. (Xinhua/Li Yahui)

Mkutano wa kwanza wa Baraza la Afrika na China juu ya Ushirikiano wa Teknolojia ya Kilimo na Viwanda ukifanyika mjini Nairobi, Kenya, Juni 24, 2025. (Xinhua/Li Yahui)

Balozi wa China nchini Kenya Guo Haiyan akitoa hotuba kwenye mkutano wa kwanza wa Baraza la Afrika na China juu ya Ushirikiano wa Teknolojia ya Kilimo na wa Viwanda mjini Nairobi, Kenya, Juni 24, 2025. (Xinhua/Li Yahui)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha