

Lugha Nyingine
Waziri wa Mambo ya Nje wa China akutana na wajumbe kutoka EU na nchi wanachama wake
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na wajumbe wa kidiplomasia nchini China kutoka Umoja wa Ulaya (EU) na nchi wanachama wake mjini Beijing, mji mkuu wa China, Juni 25, 2025. (Xinhua/Pang Xinglei)
BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amekutana na wajumbe wa kidiplomasia nchini China kutoka Umoja wa Ulaya (EU) na nchi wanachama wake jana Jumatano mjini Beijing akisema kuwa wakati mwaka huu ukiadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na EU, pande hizo mbili zenye nguvu kubwa za kiujenzi duniani leo zinapaswa kuongeza hali ya kuaminiana, kushughulikia tofauti ipasavyo, kuunganisha nguvu zao, na kuinua Uhusiano wa Kiwenzi na Kimkakati wa Pande zote kati ya China na EU katika ngazi mpya.
Wang, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ametoa pendekezo lenye vipengele vitatu kwa ajili ya maendeleo ya siku za baadaye ya uhusiano kati ya China na EU.
Kwanza, amesema, pande hizo mbili zinapaswa kudumisha kuheshimiana, hasa kwa kuheshimu kwa dhati maslahi ya makuu na masuala makubwa yanayofuatiliwa ya kila upande. Amesema kuwa kufikia muungano kamili wa kitaifa ni matarajio ya muda mrefu na jukumu la kihistoria la taifa la China, na kwamba China kamwe haitaruhusu eneo la Taiwan lijitenge na nchi mama.
Pili, amesema, pande hizo mbili zinapaswa kuzingatia msimamo uliowekwa wa ushirikiano wao, ambapo Wang amesisitiza kuwa China na EU ni washirika, si washindani, na kwa hakika si maadui.
"Hakuna migogoro ya mipaka au migogoro ya siasa za kijiografia kati ya China na EU, achilia migongano yoyote ya kimsingi ya maslahi," Wang amesema, akiongeza kuwa China inatumai kushirikiana na EU ili kuufanya ushirikiano kuwa mwelekeo wa kudumu wa uhusiano kati ya China na EU.
"Tatu, pande hizo mbili zinapaswa kuzingatia ushirikiano wa pande nyingi. China inashikilia kithabiti mfumo wa kimataifa huku Umoja wa Mataifa (UN) ukiwa msingi wake, utaratibu wa kimataifa unaoungwa mkono na sheria za kimataifa, na kanuni za msingi za uhusiano wa kimataifa kulingana na malengo na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa," Wang amesema, akiongeza kuwa China kila wakati inashikilia mazungumzo ya amani na inakataa matumizi ya nguvu.
"China na EU zinapaswa kufuata mwelekeo wa nyakati, kuongeza maelewano, kujenga hali ya kuaminiana, kutimiza hali ya kunufaishana, na kuangaza dunia kwa pamoja," Wang ameongeza.
Mkuu wa ujumbe wa EU nchini China na wajumbe wa kidiplomasia wa nchi wanachama wa EU nchini China wamesema China siku zote imekuwa mshirika muhimu wa EU, akiongeza kuwa EU inapenda kufanya kazi bega kwa bega na China kwa ajili ya siku za baadaye, kuendeleza uhusiano wa kiujenzi na tulivu kati ya EU na China, kukabiliana changamoto za kimataifa, kushikilia ushirikiano wa pande nyingi, na kuhimiza amani na usalama duniani.
Bustani ya Kimataifa ya Pump Track ya Shenyang, China: Utambulisho Mpya wa Michezo Mjini
Ukumbi wa Kuutazama Mji wa “Kilele cha Tianjin” wa China wafunguliwa rasmi kwa umma
Kuendeleza urithi wa utamaduni usioshikika wa China - ustadi wa kutengeneza chai ya Taiping Houkui
Njia mpya za uendeshaji wa droni zaanza kutumika katika Mji wa Wuhan katikati mwa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma