

Lugha Nyingine
Rais wa Kenya atoa wito wa kujizuia wakati ambapo maandamano mapya yakizuka
NAIROBI - Rais William Ruto wa Kenya ametoa wito wa utulivu na kujizuia kufuatia kuzuka kwa maandamano jana Jumatano katika miji mikubwa ya nchi hiyo.
"Nawataka wananchi wote kupinga ghasia na uharibifu wa mali ya umma. Tuna Kenya moja tu ya kujenga, na maendeleo yake yanategemea kujizuia kwa pamoja," amesema Ruto.
Wakati serikali ya Kenya bado haijatoa takwimu zozote za majeruhi au vifo, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa watu wawili wameuawa, wengine wengi kujeruhiwa, na mali ya thamani ya mamilioni kuharibiwa kwenye machafuko hayo.
Maandamano hayo yaliyozuka katika miji mbalimbali, yameshuhudia maelfu ya watu wakiingia mitaani wakiwa wamebeba mabango na kuimba nyimbo.
Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Citizen, mwanamume mmoja amefariki dunia baada ya polisi kufyatulia risasi waandamanaji katika Mji wa Matuu Kaunti ya Machakos, huku mwanafunzi akiuawa katika Mji wa Molo Kaunti ya Nakuru.
Maandamano hayo yalielezwa kuwa ni ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu Wakenya waelezee upingaji wao kwa Mswada wa Fedha wa 2024 kupitia maandamano yaliyosambaa, ambayo hatimaye yalipelekea Ruto kuuondoa bungeni mswada huo.
"Tuko hapa kuenzi wale waliouawa mwaka 2024. Ni mwaka mmoja sasa umepita tangu maandamano. Watu bado wanatekwa nyara. Inaonekana hakuna kilichobadilika," amesema Cyril Kadome, mmoja wa waandamanaji.
Biashara za kawaida zililazimika kusimama Nairobi, mji mkuu wa Kenya, na pia katika miji mingine mikubwa, ikiwemo ya Nyeri, Eldoret, Machakos, Mombasa, Kakamega, Narok, Kajiado, na Kisii.
Jijini Nairobi, maduka katika eneo la kati la biashara na maeneo mengi ya makazi yalifungwa, na vyombo vya usafiri viliwekwa nje ya barabara, huku waandamanaji wakianza kumiminika mitaani kutoka mapema saa 1:00 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki.
Awali, Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi la Kenya Douglas Kanja alisema kuwa ingawa katiba ya Kenya inaruhusu haki ya kukusanyika kwa amani na kisheria kwa raia, kitendo chochote kinzani kinakiuka sheria, na maafisa wa usalama watazuia kitendo chochote cha kuvunja amani.
Bustani ya Kimataifa ya Pump Track ya Shenyang, China: Utambulisho Mpya wa Michezo Mjini
Ukumbi wa Kuutazama Mji wa “Kilele cha Tianjin” wa China wafunguliwa rasmi kwa umma
Kuendeleza urithi wa utamaduni usioshikika wa China - ustadi wa kutengeneza chai ya Taiping Houkui
Njia mpya za uendeshaji wa droni zaanza kutumika katika Mji wa Wuhan katikati mwa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma