

Lugha Nyingine
China inaendelea kuwa "ardhi inayostawi" katika uchumi duniani: Waziri Mkuu Li
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihudhuria na kuhutubia ufunguzi wa Mkutano wa 10 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia (AIIB) mjini Beijing, mji mkuu wa China, Juni 26, 2025. (Xinhua/Liu Bin)
BEIJING - Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesema kuwa uchumi wa China unaendelea kuwa ardhi yenye kustawi katika uchumi duniani, na kwamba upanuzi na uboreshaji wa soko kubwa la China utaendelea kuwa na faida kubwa, ukitoa fursa nyingi zaidi za biashara na uwekezaji kwa nchi zingine.
Akizungumza jana Alhamisi kwenye hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa 10 wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia (AIIB) mjini Beijing, Li amesisitiza tena kuwa China itafungua mlango kwa kiwango cha juu na itaendelea kushiriki kwa kina kwenye uchumi duniani, hatua ambayo inatarajiwa kutoa fursa mpya za maendeleo duniani kote.
Li amesema kuwa wakati AIIB ilipozinduliwa, Rais Xi Jinping wa China alipendekeza kuifanya AIIB kuwa "aina mpya ya benki ya maendeleo ya pande nyingi iliyo ya kitaaluma, yenye ufanisi na safi."
“Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, idadi ya pande wanachama wa AIIB imeongezeka kutoka 57 hadi 110,” Li amesema, akiipongeza benki hiyo kwa kuhimiza nchi wanachama wake kujiendeleza kwa pamoja, kuanzisha mifumo mipya ya usimamizi wa mambo ya fedha duniani, na kuweka mfano mpya kwa ushirikiano wa kimataifa wa pande nyingi.
Kuhusu maendeleo ya baadaye ya benki hiyo, Li amesema katika kukabiliana na changamoto za ukuaji uchumi duniani, AIIB inapaswa kuongeza uungaji mkono wake kwa maendeleo ya nchi wanachama wake.
"AIIB inapaswa kutoa ufadhili wa kiwango cha juu, wa gharama nafuu ambao unakidhi mahitaji mbalimbali ya maendeleo ya nchi wanachama wake, kuwezesha mawasiliano ya utaalamu na uzoefu, na kusaidia kuimarisha msukumo wao wa ndani wa ukuaji," Li amesema.
Aidha, Waziri Mkuu huyo amesisitiza kwamba AIIB inahitaji kuhimiza mazungumzo na uratibu zaidi wa kimataifa na kuchukua jukumu bora kama jukwaa jipya la pande nyingi katika kukabiliana changamoto za usimamizi wa dunia.
"China inapenda kushirikiana na pande zote kuunga mkono AIIB katika kuanza muongo mpya wa utukufu, na kutoa mchango mkubwa zaidi katika kuendeleza maendeleo endelevu ya pande wanachama wake na kuhimiza ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu," Li amesema.
Ukiwa unafanyika chini ya kaulimbiu ya "Kuunganisha kwa Maendeleo, Kushirikiana kwa Ustawi," mkutano wa mwaka huu umeandaliwa kwa pamoja na Wizara ya Fedha ya China, Serikali ya Beijing, na AIIB.
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihudhuria na kuhutubia ufunguzi wa Mkutano wa 10 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia (AIIB) mjini Beijing, mji mkuu wa China, Juni 26, 2025. (Xinhua/Ding Haitao)
Bustani ya Kimataifa ya Pump Track ya Shenyang, China: Utambulisho Mpya wa Michezo Mjini
Ukumbi wa Kuutazama Mji wa “Kilele cha Tianjin” wa China wafunguliwa rasmi kwa umma
Kuendeleza urithi wa utamaduni usioshikika wa China - ustadi wa kutengeneza chai ya Taiping Houkui
Njia mpya za uendeshaji wa droni zaanza kutumika katika Mji wa Wuhan katikati mwa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma