Mjumbe wa China atoa wito wa kufanya juhudi za kushikilia mfumo wa kimataifa ambao kiini chake ni Umoja wa Mataifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 27, 2025

Fu Cong, mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa  akitoa hotuba kwenye shughuli ya Baraza Kuu ya kuadhimisha miaka 80 tangu kutiwa saini kwa Katiba ya Umoja wa Mataifa   katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Juni 26, 2025. (Xinhua/Xie E)

UMOJA WA MATAIFA - Fu Cong, Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa jana Alhamisi alipotoa hotuba kwenye shughuli ya Baraza Kuu ya kuadhimisha miaka 80 tangu kutiwa saini kwa Katiba ya Umoja wa Mataifa alitoa wito wa kufanya juhudi za kushikilia mfumo wa kimataifa ambao kiini chake ni Umoja wa Mataifa.

Fu amesema, katika miaka 80 iliyopita, kufuatia ushindi mkubwa wa Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti, mkutano wa San Francisco kwa kauli moja ulipitisha Katiba ya Umoja wa Mataifa, ukiweka jiwe la msingi wa ushirikiano wa pande nyingi, kuthibitisha kanuni za kimsingi za uhusiano wa kimataifa, na kuelekeza njia ya kusonga mbele kwa binadamu.

Amezitaka nchi mbalimbali kwa pamoja kulinda matokeo ya ushindi wa Vita vya Pili vya Dunia na kukataa maneno au vitendo vyovyote vya makosa vinavyokusudia kupotosha historia.

"Tunapaswa kushikilia kithabiti mfumo wa kimataifa ambao kiini chake ni Umoja wa Mataifa, kuhifadhi utaratibu wa kimataifa unaowekwa kwenye msingi wa sheria za kimataifa, na kuhifadhi mfumo wa biashara ya pande nyingi unaofuata sheria," ameongeza.

Balozi Fu ametoa wito wa kufanya juhudi za kutii nia na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa na kuheshimu mamlaka ya nchi, uhuru, na ukamilifu wa ardhi wa nchi zote .

"Tunapaswa kutetea matumaini ya usalama wa pamoja, jumuishi, wa ushirikiano na endelevu, kudhamiria kwenye kutatua migogoro kwa njia ya amani, na kupinga kutumia ovyo nguvu ya kisilaha au kutoa tishio la kutumia nguvu ya kisilaha" ameongeza.

Amesisitiza haja ya kutekeleza ushirikiano wa kweli wa pande nyingi, kuwa na mshikamano kwa kuunga mkono Umoja wa Mataifa kuonesha umuhimu wake katika mambo ya kimataifa, kuhimiza utekelezaji wa Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu, na kufanya juhudi za pamoja za kukabiliana na changamoto duniani.

Balozi Fu amesema, “China ilikuwa nchi ya kwanza kutia saini kwenye Katiba ya Umoja wa Mataifa”, China itaendelea kufanya vitendo halisi vya kufuata ahadi yake kwa Katiba ya Umoja wa Mataifa, na kufanya juhudi zisizolegea kwa ajili ya kulinda amani na maendeleo ya Dunia. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres akizungumza kwenye  shughuli ya Baraza Kuu ya kuadhimisha miaka 80 tangu kutiwa saini kwa Katiba ya Umoja wa Mataifa   katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Juni 26, 2025. (Xinhua/Xie E)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha