Takriban 20 wauawa katika tukio la kukanyagana kwenye shule ya sekondari mjini Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 27, 2025

Watu waliojeruhiwa wakibebwa kuingizwa kwenye gari la wagonjwa mjini Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Juni 25, 2025. (Str/Xinhua)

Watu waliojeruhiwa wakibebwa kuingizwa kwenye gari la wagonjwa mjini Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Juni 25, 2025. (Str/Xinhua)

BANGUI - Watu takriban 20 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika tukio la kukanyagana lililosababishwa na mlipuko wa transfoma ya umeme kwenye Shule ya Sekondari ya Juu ya Barthelemy Boganda mjini Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), Jumatano, Bunge la Taifa la nchi hiyo limesema katika taarifa iliyotolewa jana Alhamisi.

Bunge hilo limesema mlipuko huo ulisababisha mtafaruku miongoni mwa watahiniwa wa mtihani, ikisababisha tukio hilo wakati wakijaribu kukimbia hatari na kwamba waathiriwa wamepelekwa katika vituo mbalimbali vya matibabu katika mji mkuu huo.

"Tukiwa katikati ya mtihani wakati tuliposikia mlipuko mkubwa, kila mmoja akaanza kukimbia. Wanafunzi wenzangu kadhaa walianguka na kushindwa kuinuka," amesema Rufin Pandama, mwanafunzi aliyekuwepo eneo la tukio.

Vituo viwili vya mtihani katika shule hiyo vilikuwa vimepangiwa watahiniwa jumla ya 5,311 na hadi sasa, ripoti rasmi na ya kina kuhusu vifo na majeruhi bado haijatolewa.

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa ajali hiyo imegharimu maisha ya wanafunzi takriban 29.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatano na Wizara ya Elimu ya nchi hiyo, kufuatia hitilafu ya kiufundi mapema siku hiyo, timu ya Shirika la Energie Centrafricaine (ENERCA) ilitumwa kufanya kazi ya ukarabati na kwamba mlipuko huo umetokea wakati nishati ilikuwa ikirejeshwa.

Kwenye hotuba ya video, Rais Faustin-Archange Touadera wa CAR ametangaza kipindi cha siku tatu cha maombolezo ya kitaifa kuanzia jana Alhamisi, katika kuwaomboleza watu waliofariki kwenye mlipuko huo mbaya.

Rais huyo ametoa salamu za rambirambi kwa familia zilizofiwa, walimu, na jumuiya ya kielimu iliyoguswa na msiba huo, na kutangaza kuanzishwa kwa uchunguzi wa kisheria ili kujua chanzo hasa cha tukio hilo na wale waliohusika. 

Picha hii iliyopigwa Juni 25, 2025 ikionyesha watu wakiwa wamekusanyika mbele ya Shule ya Sekondari ya Juu ya Barthelemy Boganda, mahali palipotokea tukio la kukanyagana, mjini Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati. (Str/Xinhua)

Mtu aliyejeruhiwa akibebwa kuingizwa kwenye gari la wagonjwa mjini Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Juni 25, 2025. (Str/Xinhua)

Mtu aliyejeruhiwa akibebwa kuingizwa kwenye gari la wagonjwa mjini Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Juni 25, 2025. (Str/Xinhua)

Watu waliojeruhiwa wakibebwa kuingizwa kwenye gari la wagonjwa mjini Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Juni 25, 2025. (Str/Xinhua)

Watu waliojeruhiwa wakibebwa kuingizwa kwenye gari la wagonjwa mjini Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Juni 25, 2025. (Str/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha