Mkoa wa Guangdong, China wadhamiria kujenga kundi la viwanda vya zana na vifaa vya hali ya juu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 01, 2025
Mkoa wa Guangdong, China wadhamiria kujenga kundi la viwanda vya zana na vifaa vya hali ya juu
Mfanyakazi akipangilia vigezo kabla ya kuchomelea kwenye Kampuni ya Otomesheni ya Roboti ya Guangdong Lyric mjini Huizhou, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, Juni 27, 2025. (Xinhua/Deng Hua)

GUANGZHOU - Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China umekuwa ukiimarisha miji yake mhimili ikiwemo ya Guangzhou, Shenzhen, Foshan na Dongguan katika shughuli za utengenezaji wa zana na vifaa vya kisasa, na kufanya juhudi za kujenga kundi la viwanda vya utengenezaji wa zana na vifaa vya hali ya juu.

Mwaka 2024, mapato ya mkoa huo kwenye viwanda vya utengenezaji wa zana na vifaa vya hali ya juu yalifikia yuan bilioni 390.565 (dola za kimarekani bilioni 54.5) huku faida ya jumla ikisimama katika yuan bilioni 18.873 (dola za kimarekani bilioni 2.63).

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha