Ushirikiano wa SCO unaendelea kwa nguvu na unatoa msukumo kwa uchumi wa dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 28, 2025

BEIJING – Kikihimizwa na kushamiri kwa manunuzi na utalii wa kuvuka mpaka, Kituo cha Ushirikiano cha Kimataifa cha China-Kazakhstan cha Horgos katika wiki za hivi karibuni kimeshuhudia pilika za watu wanaovuka mpaka na idadi ya wanaovuka kila siku kuwa zaidi ya watu 30,000.

Hadi kufikia Julai 11, zaidi ya watu milioni 5 wa kuvuka mpaka walikuwa walipita kwenye kituo cha kilomita za mraba 5.6 mwaka huu, likiwa ni ongezeko la asilimia 73 kwa mwaka. Kituo hiki kipo Horgos kaskazini magharibi mwa China kwenye Mkoa wa Xinjiang na eneo lengine liko upande wa Kazakhstan.

Watalii wanatembelea duka lisilotozwa ushuru katika Kituo cha Ushirikiano wa Kimataifa cha Mpakani cha Horgos kwenye mpaka kati ya China na Kazakhstan huko Horgos, mkoani Xinjiang China, Julai 26, 2024. (Xinhua/Ding Lei)

Likiwa ni eneo la vielelezo vya ushirikiano wa kikanda chini ya mfumo wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO), kituo hicho kimeshuhudia kukua kwa uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya wanachama wa jumuiya hiyo, ambayo ilianzishwa miaka 24 iliyopita na China, Russia, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan na Uzbekistan.

Jumuiya hiyo ikiwa na nchi 10 wanachama, nchi 2 waangalizi na washirika 14 wa mazungumzo, sasa inawakilisha karibu nusu ya idadi ya watu duniani, robo ya ardhi ya nchi kavu na karibu robo ya pato la dunia. Tangu kuanzishwa kwake mwaka wa 2001, SCO imekua na kuwa jumuiya kubwa ya kikanda inayochangia uhakika na uhai wa hali ya uchumi wa dunia ambayo mara nyingi ina utatanishi.

Viongozi kutoka nchi za Asia, Ulaya na Afrika watakusanyika mjini Tianjin kaskazini mwa China kati ya Agosti 31 na Septemba 1 kwenye mkutano mkubwa zaidi wa kilele wa SCO katika historia, unaotarajiwa kuweka ramani ya maendeleo ya baadaye ya jumuiya hiyo na kuchangia uhai zaidi katika uchumi wa dunia.

Picha hii iliyopigwa Agosti 22, 2025 inaonyesha nguzo za taa zilizopambwa kwa mabango ya Mkutano ujao wa 2025 wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) katika eneo jipya la Binhai, mjini Tianjin China. (Xinhua/Zhao Zishuo)

Mtalii anatembelea duka lisilotoza ushuru katika Kituo cha Ushirikiano wa Kimataifa cha Mpakani cha Horgos, Mkoani Xinjiang China, Julai 26, 2024. (Xinhua/Ding Lei)

Mtalii anatembelea duka lisilotoza ushuru katika Kituo cha Ushirikiano wa Kimataifa cha Mpakani cha Horgos, Mkoani Xinjiang China, Julai 26, 2024. (Xinhua/Ding Lei)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha