

Lugha Nyingine
Ndugu wa Taiwan waalikwa kwenye gwaride la siku ya ushindi mjini Beijing
Msemaji wa Ofisi ya Mambo ya Taiwan ya Baraza la Serikali la China Bibi Zhu Fenglian, akiongea kwenye mkutano wa kawaida na wanahabari mjini Beijing, China, Agosti 27, 2025. (Xinhua/Chen Yehua)
BEIJING -- Watu kutoka sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na watu wa Taiwan, wataalikwa kutazama gwaride kubwa la kijeshi la China la Siku ya ushindi, lililopangwa kufanyika Septemba 3 katika uwanja wa Tian'anmen mjini Beijing.
Msemaji wa Ofisi ya Mambo ya Taiwan ya Baraza la serikali la China Bibi Zhu Fenglian, amesema kwenye mkutano na wanahabari kwamba mwaka huu ni kumbukumbu ya miaka 80 ya ushindi wa vita vya watu wa China vya kupambana na uvamizi wa Japan na Vita vya dunia vya kupinga Ufashisti, na miaka 80 ya Taiwan kujitoa kutoka utawala wa kikoloni.
Bibi Zhu amesema vita vya kupambana na uvamizi wa Japan ni juhudi zilizofanywa na taifa zima la China, pamoja na watu wote wa China, wakiwemo ndugu wa Taiwan waliojitolea mhanga na kutoa mchango mkubwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma