China yahimiza Israel kusitisha mara moja operesheni ya kijeshi huko Gaza

(CRI Online) Agosti 28, 2025

Naibu mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Geng Shuang ametoa hotuba katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Palestina na Israel akihimiza Israel kusitisha mara moja operesheni yake ya kijeshi katika ukanda wa Gaza.

Bw. Geng amesema mgogoro wa Gaza umedumu kwa karibu siku 700 na ukanda hiyo kwenye hali ngumu kwa muda mrefu, huku watu milioni 2 wa Gaza wakikwamwa kwenye maafa makubwa ya kibinadamu. Jumuiya ya kimataifa inatakiwa kufanya juhudi zote kuzuia hali kuzidi kuwa mbaya.

Bw. Geng amesema mabavu hayawezi kuleta usalama na nguvu haiwezi kuleta amani. Israel inaendelea kuongeza mashambulizi ya kijeshi yakisababisha vifo vya raia wengi wa kawaida. Shambulizi lililofanywa tarehe 25 dhidi ya hospitali ya Nasser limesababisha vifo vya watu zaidi ya 20 wa kawaida.

Amesema China inapinga vitendo vyote vya kuwadhuru raia wa kawaida, kuharibu vifaa vya kiraia na kukiuka sheria za kimataifa, huku ikiihimiza Israel kusitisha mara moja operesheni ya kijeshi katika ukanda wa Gaza, na kusimama kuchukua hatua za hatari zinazoweza kuzidisha hali ya wasiwasi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha