Nchi 14 wajumbe wa Baraza la Usalama la UM zatoa wito wa kukabiliana na njaa Gaza mara moja

(CRI Online) Agosti 28, 2025

Guyana na Slovenia, zikiwa waratibu wasio rasmi wa sehemu ya "Misukisuko na Njaa" ya Baraza la Usalama la UM, pamoja na wajumbe wote wa Baraza la Usalama isipokuwa Marekani, wametoa taarifa ya pamoja katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa wakielezea mshtuko na wasiwasi juu ya ripoti ya Umoja wa Mataifa kuthibitisha njaa katika Ukanda wa Gaza. Hii ni mara ya kwanza kwa njaa kuthibitishwa rasmi katika eneo la Mashariki ya Kati.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa watu wengi zaidi wanakufa kila siku kutokana na utapiamlo huko Gaza, ikiwa ni pamoja na idadi kubwa ya watoto. Njaa hiyo inatarajiwa kuenea hadi Deir al-Balah na Khan Younis mwishoni mwa Septemba. Takriban watu milioni 1.5 katika Ukanda wa Gaza wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, na watoto 132,000 wanatarajiwa kukabiliwa na utapiamlo mkali ifikapo Juni mwaka 2026, na elfu 41 kati yao wakiwa katika hatari ya kifo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha