Zaidi ya watu 82,000 hawajulikani walipo barani Afrika

(CRI Online) Agosti 28, 2025

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) imesema, zaidi ya watu 82,000 kwa sasa hawajulikani walipo kote barani Afrika kutokana na vita na ghasia.

Mkurugenzi wa ICRC Kanda ya Afrika Patrick Youssef amesema katika taarifa iliyotolewa jana katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi kuwa, idadi hii inawakilisha sehemu ndogo tu ya wale ambao wametoweka.

ICRC na Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu waliwezesha kuunganishwa tena kwa familia 755 katika bara hilo mwaka 2024, na kutoa habari za uhakika za sehemu walipo ndugu wa familia 5,083.

Kulingana Shirika hilo, mzozo nchini Sudan ndio sababu kuu ya ongezeko hili, na zaidi ya maombi 7,700 ya kusaidia kupatikana kwa mtu aliyepotea yanahusiana na mzozo huo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha