Mfanyabiashara haramu wa pembe za faru akamatwa nchini Kenya

(CRI Online) Agosti 28, 2025

Mfanyabiashara haramu wa wanyamapori ambaye aliorodheshwa katika Tangazo Jekundu la Polisi wa Kimataifa na aliyewahi kuhukumiwa katika mahakama kutokana na kumiliki pembe za wanyamapori, amekamatwa pamoja na mwenzake nchini Kenya kwa kumiliki pembe za faru kinyume na sheria.

Shirika la Kuhudumia Wanyamapori la Kenya (KWS) limesema katika taarifa yake kwamba, raia wa Kenya anayeitwa Feisal Mohamed Ali na mwenzake walikamatwa katika mji wa pwani wa Mombasa jumanne wiki hii wakiwa na vipande viwili vya pembe za faru zenye uzito wa kilogram 2.2.

Mkurugenzi mkuu wa KWS Erustus Kanga amesema, kukamatwa kwa wahalifu hao kunaonesha tena nia ya Kenya ya kupambana na uhalifu dhidi ya wanyamapori na kuvunja mitandao ya kisasa ya usafirishaji haramu wa wanyamapori.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha