

Lugha Nyingine
Wataalamu wa China wawasili Tanzania Zanzibar kuendeleza mradi wa kudhibiti kichocho
(CRI Online) Agosti 28, 2025
Kundi la tatu la wataalamu wa China kwa ajili ya awamu ya pili ya mradi wa kutokomeza kichocho unaofadhiliwa naChina, wamewasili kisiwani Unguja, Tanzania Zanzibar, wakiashiria ukurasa mpya katika ushirikiano wa pande mbili kuhusu afya ya umma.
Baada ya kuwasili, timu hiyo ya wataalamu ilifanya mazungumzo na wadau muhimu, zikiwemo Wizara ya Afya ya Zanzibar, Wizara ya Maji, Nishati na Madini, Taasisi ya Utafiti Zanzibar na Mradi wa Magonjwa ya Kitropiki Yaliyosahaulika katika visiwa vya Pemba na Unguja, pamoja na Wizara ya Afya ya Pemba.
Kwa mujibu wa kiongozi mpya wa kikundi hicho, Wang Wei, timu hiyo ilikagua mazingira ya maji na maeneo ya vyanzo vya ufuatiliaji wa kichocho ili kutathmini mazingira ya huko na maendeleo yaliyopatikana.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma