

Lugha Nyingine
Waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini aeleza wasiwasi kuhusu nyongeza ya ushuru
(CRI Online) Agosti 28, 2025
Waziri wa Uhusiao wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini, Ronald Lamola jana Jumatano amesema, ingawa serikali ya nchi hiyo ina matumaini mazuri kuhusu mazungumzo kuhusu nyongeza ya ushuru wa asilimia 30 kwa bidhaa zinazoingizwa na Marekani kutoka Afrika Kusini yanayoendelea, lakini matokeo ya mazungumzo hayo bado hayajulikani.
Lamola amesisitiza kuwa, Afrika Kusini sio nchi pekee inayokabiliwa na hatua hiyo ya Marekani, akisema nchi nyingine zikiwemo Brazil, Uswisi na India pia zimekumbwa na mpango wa Marekani wa kuongeza ushuru, na kusema serikali ya Afrika Kusini itafanya juhudi na kuendelea na mazungumzo, ili kujaribu matokeo mazuri.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma