Mkulima aleta matunda ya Asia nchini Cameroon

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 28, 2025

Wafanyakazi wanabeba matunda yaliyovunwa kutoka kwenye shamba la Arnold Kogaing huko Souza, Mkoani Littoral Cameroon, Agosti 20, 2025. (Xinhua/Kepseu)

Wafanyakazi wanabeba matunda yaliyovunwa kutoka kwenye shamba la Arnold Kogaing huko Souza, Mkoani Littoral Cameroon, Agosti 20, 2025. (Xinhua/Kepseu)

YAOUNDE -- Kwenye shamba la matunda la hekta 10 katika eneo la Souza Mkoani Littoral nchini Cameroon, Arnold Kogaing anachuma matunda na kuyapakia kwenye mifuko ya ununuzi.

Bwana huyo mwenye umri wa miaka 35 hakuwahi kufikiria kwamba siku moja angekuwa mkulima wa matunda ya Asia mara moja yaliyokuwa yakipatikana tu kwa kupitia uagizaji kutoka nje, hadi mwaka 2008 aliposomea uhandisi wa mashine nchini China alibadilisha mtazamo wake. Katika miaka yake ya uanafunzi nchini China, Kogaing alijifunza kuhusu mbinu za kilimo na usimamizi wa matunda, hasa mbinu za kutumia mabanda ya kilimo. Alisema "siku zote nimekuwa nikipenda matunda. Nilitembelea mashamba nchini China. Nilijifunza na kujisemea, 'Kwa nini nisilime matunda hayo nchini Cameroon?'"

Baada ya kumaliza masomo yake ya chuo kikuu, baba huyo wa watoto wawili alirudi Cameroon, akiwa na ujuzi muhimu wa kilimo cha matunda ya Asia. Katika eneo lenye joto la Souza, ambako mwanga wa jua, joto, na maji mengi huchanganyikana na kuleta paradiso ya kitropiki, Bw. Kogaing aligundua kwamba mbegu inayopandwa mara nyingi huchipuka kwa kasi ya ajabu. Ndio maana mwaka 2019, alianza kulima aina mbalimbali za matunda, ikiwa ni pamoja na matunda ya dragon fruit, longan, jackfruit, lychee, cheri, matikiti ya China, na matunda ya pasheni.

Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2020, Bw. Kogaing alivuna mavuno yake ya kwanza, na kuleta kwa mara ya kwanza aina ya matunda ya Asia nchini Cameroon.

Hata hivyo, ilikuwa ni vigumu kwa matunda hayo kupendwa kwenye soko la ndani, hii ilimbidi Bw. Kogaing ategemee wahamiaji kutoka Asia kama wateja wake wa kwanza. Bw. Kigaing alisema, “Baada ya muda, tulianza kuruhusu watu kuonja ili kuwafahamisha kuhusu matunda hayo na manufaa yake. Mara baada ya watu wa Cameroon kuonja, waliyapenda sana. Leo, tuna idadi kubwa ya watu wa Cameroon ambao tayari wanafahamu matunda hayo na manufaa yake."

Bw. Kogaing pia alisema kwenye shamba lake, “Leo, tuna takriban aina 18 za matunda. Kwa wastani, tunaweza kuzalisha tani nne hadi tano za matunda na mboga kila mwezi.”

Picha iliyopigwa Agosti 20, 2025 inamwonyesha Arnold Kogaing akitambulisha matunda ya dragon fruit katika shamba lake huko Souza, Mkoani Littoral Cameroon. (Xinhua/Kepseu)

Picha iliyopigwa Agosti 20, 2025 inamwonyesha Arnold Kogaing akitambulisha matunda ya dragon fruit katika shamba lake huko Souza, Mkoani Littoral Cameroon. (Xinhua/Kepseu)

Mfanyakazi anakula tunda la dragon fruit katika shamba la Arnold Kogaing huko Souza, Mkoani Littoral Cameroon, Agosti 20, 2025. (Xinhua/Kepseu)

Mfanyakazi anakula tunda la dragon fruit katika shamba la Arnold Kogaing huko Souza, Mkoani Littoral Cameroon, Agosti 20, 2025. (Xinhua/Kepseu)

Wafanyakazi wanasafisha matunda ya dragon fruit kabla ya kuyahifadhi kwenye mabeseni kwenye  shamba la Arnold Kogaing huko Souza, Mkoani Littoral Cameroon, Agosti 20, 2025. (Xinhua/Kepseu)

Wafanyakazi wanasafisha matunda ya dragon fruit kabla ya kuyahifadhi kwenye mabeseni kwenye shamba la Arnold Kogaing huko Souza, Mkoani Littoral Cameroon, Agosti 20, 2025. (Xinhua/Kepseu)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha