Umoja wa Mataifa: Mji wa El Fasher wa Sudan wawa kitovu cha mateso kwa watoto

(CRI Online) Agosti 28, 2025

Ofisi ya Uratibu wa Mambo ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema jana Jumatano kuwa ukiwa umezingirwa kwa siku 500, mji wa El Fasher wa jimbo la Darfur Kaskazini la Sudan umekuwa kitovu cha mateso kwa watoto na hali mbaya katika jimbo hilo inaendelea kuzorota kwa kasi.

Shirika la kuhudumia watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) limesema zaidi ya watoto elfu 10 huko El Fasher wamekumbwa na utapiamlo mbaya tangu Januari mwaka huu, karibu mara mbili ya idadi ya mwaka jana. Shirika hilo pia limesema kuwa kuzingirwa na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) dhidi ya El Fasher, kumekata kabisa njia za usambazaji wa misaada huko. Vituo vya afya na timu za utoaji wa chakula zinazohamishika zimelazimika kusimamisha huduma zao, na hivyo kuacha takriban watoto elfu sita wakiwa na utapiamlo mkali na kutokuwa na matibabu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha