China iko tayari kuimarisha ushirikiano wa kimkakati wa kina na Brazil

(CRI Online) Agosti 29, 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema, nchi hiyo iko tayari kuboresha uaminifu wa kimkakati na Brazil, kuunga mkono kithabiti kila upande na kuimarisha ushirikiano wa kimkakati katika maeneo mbalimbali kati ya nchi hizo mbili.

Wang amesema hayo wakati akizungumza kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil Mauro Vieira hapo jana. Amesema rais wa China Xi Jinping na wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva kwa pamoja wametoa mwongozo muhimu wa kimkakati kwa ajili ya ujenzi wa jumuiya ya pamoja ya China na Brazil yenye mustakabali wa pamoja.

Kwa upande wake, Vieira amesema, Brazil ina matarajio makubwa ya kuimarisha mawasiliano na uratibu na China na pande husika, kutafiti njia za kuunga mkono mfumo wa biashara ya pande nyingi, na kuboresha mageuzi ya Shirika la Biashara Duniani (WTO).

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha