

Lugha Nyingine
Viongozi kutoka nchi mbalimbali kuhudhuria kumbukumbu ya ushindi wa China dhidi ya uvamizi wa Japan
Mkutano wa kwanza na wanahabari kuhusu maandalizi ya maadhimisho ya siku ya ushindi ulifanyika kwenye Kituo cha vyombo vya habari cha Kumbukumbu ya Miaka 80 ya Ushindi wa Watu wa China kupambana na uvamizi wa Japan na Ushindi wa Dunia dhidi ya Ufashisti mjini Beijing, China, Agosti 28, 2025. (Xinhua/Jin Liangkuai)
Rais wa China Xi Jinping atapokea viongozi kutoka nchi 26 wakati wa gwaride la kumbukumbu ya miaka 80 ya ushindi wa China dhidi ya uvamizi wa Japan na ushindi wa dunia dhidi ya Ufashisti litakalofanyika wiki ijayo katika Uwanja wa Tian'anmen mjini Beijing.
Kwa mujibu wa orodha ya wageni iliyotangazwa na Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje ya China Hong Lei, miongoni mwa wageni watakaohudhuria sherehe hiyo ni rais wa Russia Vladmir Putin, kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, pamoja na viongozi kutoka Cambodia, Vietnam, Laos, Indonesia, Malaysia, Mongolia, Pakistan, Belarus, Serbia, Iran, na Cuba.
Hong amesema, ushindi wa China katika vita dhidi ya uvamizi wa Japan miaka 80 iliyopita ulizihamasisha nchi zilizotawaliwa na wakoloni kuongeza juhudi za kujipatia uhuru.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma