Mapigano mapya yazuka katika vikosi vya serikali na makundi ya upinzani nchini Sudan Kusini

(CRI Online) Agosti 29, 2025

Mapigano makali kati ya Jeshi la Ulinzi la Sudan Kusini na kundi la upinzani la SPLA-IO la nchini humo yameendelea kwa siku mbili katika mikoa ya Ikweta ya Kati na Upper Nile nchini humo.

Msemaji wa kundi la SPLA-IO Lam Paul Gabriel amesema kupitia ukurasa wake wa Facebook hapo jana kwamba, wapiganaji wa kundi hilo walizuia shambulizi lililofanywa na Jeshi la Sudan Kusini pembezoni mwa Mathiang, na kusababisha mapigano makali katikati ya mji na kaunti ya Longechuk.

Pia amesema, mapigano yametokea kuanzia jumatano baada ya kundi hilo kuzuia mashambulizi mawili ya Jeshi la Sudan Kusini katika maeneo ya Jamara Saba na Limuro katika kaunti ya Lainya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha