Rwanda yapokea kundi la kwanza la wahamiaji 7 waliofukuzwa na Marekani

(CRI Online) Agosti 29, 2025

Msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo amesema, nchi hiyo imepokea wahamiaji haramu 7 waliofukuzwa kutoka Marekani, ikiwa ni kundi la kwanza la wahamiaji kuwasili chini ya makubaliano ya hivi karibuni kati ya Rwanda na Marekani ya kuwapatia makazi mapya wahamiaji hao.

Akizungumza na wanahabari hapo jana, Makolo amesema, wahamiaji hao waliwasili katikati ya mwezi huu, na kwamba Shirika la Kimataifa la Uhamiaji na huduma za kijamii za nchini humo zinaendelea kufuatilia hali zao za maisha. Amesema wahamiaji wanne kati yao wameamua kuanza maisha mapya nchini Rwanda, huku watatu waliosalia wakidhamiria kurejea katika nchi zao za asili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha