Rais Xi asema Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) inabeba majukumu makubwa zaidi ya amani na maendeleo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 01, 2025

Rais Xi Jinping wa China akihutubia tafrija ya kuwakaribisha wageni wa kimataifa katika Kituo cha Maonyesho cha Meijiang mjini Tianjin, China, Agosti 31, 2025.  Rais Xi na mkewe Bibi Peng Liyuan, Jumapili waliandaa tafrija ya kuwakaribisha wageni wa kimataifa waliokuja mjini Tianjin kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (Xinhua/Xie Huanchi)

TIANJIN - Rais Xi Jinping wa China amesema Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) inabeba majukumu makubwa zaidi ya kulinda amani na utulivu wa kikanda, na kuhimiza maendeleo ya nchi mbalimbali katika dunia yenye sintofahamu zinazoongezeka na mabadiliko ya haraka.

Rais Xi ameyasema hayo mjini Tianjin kwenye tafrija ya kuwakaribisha wageni wa kimataifa ambao wamekuja nchini China kuhudhuria Mkutano wa mwaka huu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai ulioanza Jumapili na kumaliza Jumatatu.

Kabla ya tafrija hiyo, Rais Xi pamoja na mkewe Bibi Peng Liyuan waliwakaribisha wageni hao.

Akihutubia tafrija hiyo Rais Xi alionyesha imani yake kwamba kutokana na juhudi za pamoja za pande zote, mkutano huo utakuwa na mafanikio kamili, na kwamba Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai ina uhakika wa kuwa na jukumu kubwa zaidi na kufikia maendeleo zaidi, kutoa mchango mkubwa katika kuimarisha umoja na ushirikiano kati ya nchi wanachama, kuunganisha nguvu ya nchi za kusini duniani na kuhimiza maendeleo zaidi ya ustaarabu wa binadamu.

Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai ilianzishwa mjini Shanghai Juni 2001, na sasa imepanuka kutoka nchi sita wanachama waanzilishi na kuwa familia ya nchi 26, kati ya hizo 10 ni nchi wanachama, nchi 2 waangalizi, na nchi 14 washirika wa mazungumzo yanayohusisha Asia, Ulaya na Afrika.

Masoko makubwa yanayoibuka na nchi zinazoendelea China, Russia na India zikiwa ni miongoni mwa wanachama wake, Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai ina karibu nusu ya idadi ya watu duniani na robo ya uchumi wa dunia.

Mkutano wa kilele wa Tianjin ni mkutano mkubwa zaidi wa mwaka wa Jumuiya hiyo. Nchi wanachama zinatarajiwa kupitisha nyaraka muhimu, ikiwa ni pamoja na mkakati wa maendeleo wa Jumuiya hiyo katika muongo mmoja ujao.

Rais Xi Jinping wa China akihutubia tafrija ya kuwakaribisha wageni wa kimataifa kwenye Kituo cha Maonyesho cha Meijiang mjini Tianjin, China, Agosti 31, 2025. (Xinhua/Ding Haitao)

Rais Xi Jinping wa China akihutubia tafrija ya kuwakaribisha wageni wa kimataifa kwenye Kituo cha Maonyesho cha Meijiang mjini Tianjin, China, Agosti 31, 2025. (Xinhua/Ding Haitao)

Rais Xi Jinping wa China akihutubia tafrija ya kuwakaribisha wageni wa kimataifa katika Kituo cha Maonyesho cha Meijiang mjini Tianjin, China, Agosti 31, 2025. (Xinhua/Ding Haitao)

Rais Xi Jinping wa China akihutubia tafrija ya kuwakaribisha wageni wa kimataifa katika Kituo cha Maonyesho cha Meijiang mjini Tianjin, China, Agosti 31, 2025. (Xinhua/Ding Haitao)

Rais Xi Jinping wa China na mkewe Bibi Peng Liyuan, wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya tafrija ya kuwakaribisha kwenye Kituo cha Maonyesho cha Meijiang mjini Tianjin, China, Agosti 31, 2025. (Xinhua/ Huang Jingwen)

Rais Xi Jinping wa China na mkewe Bibi Peng Liyuan, wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya tafrija ya kuwakaribisha kwenye Kituo cha Maonyesho cha Meijiang mjini Tianjin, China, Agosti 31, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha