Maadhimisho ya miaka 80 ya ushindi wa Vita ya Watu wa China dhidi ya uvamizi wa Japan kuanza kesho kwenye Uwanja wa Tian'anmen

(CRI Online) Septemba 02, 2025

Maadhimisho ya miaka 80 ya ushindi wa Watu wa China kupambana dhidi ya Uvamizi wa Japan na Vita ya Dunia ya Kupinga Ufashisti, utakaojumuisha gwaride la kijeshi, utaanza kesho saa 3 asubuhi kwa saa za Beijing kwenye Uwanja wa Tian'anmen mjini Beijing.

Rais Xi Jinping wa China atahutubia mkutano na kukagua gwaride.

Kesho saa 2 jioni kwa saa za Beijing, tamasha la kumbukumbu litafanyika katika Jumba kuu la Mikutano ya Umma la Beijing, ambapo rais Xi atahudhuria tamasha hilo. Maadhimisho hayo yote yatatangazwa moja kwa moja na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) na kupitia tovuti ya Xinhuanet.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha