

Lugha Nyingine
Mazungumzo ya ustaarabu kati ya China na Misiri yafanyika mjini Cairo
Mazungumzo mapya ya ustaarabu kati ya Misri na China yamefanyika kwenye Jumba la Makumbusho la kitaifa la Ustaarabu wa Misri (NMEC) mjini Cairo, yakiangazia urithi wa ustaarabu wa Mto Nile wa Misri na Mto Changjiang wa China.
Mazungumzo hayo yenye kauli mbiu ya “Wakati mto Changjiang unapokutana na Mto Nile” iliandaliwa kwa pamoja na Jumba la Makumbusho la kitaifa la Misri na Idara ya utamaduni na utalii kutoka mji wa Chongqing, China.
Ofisa mkuu mtendaji wa Jumba la Makumbusho la kitaifa la Ustaarabu wa Misri Bw. El-Tayeb Abbas, amesema kwenye hafla ya ufunguzi kuwa mkutano huo ni zaidi ya kukutana kwa mito miwili mirefu zaidi duniani, kwa kuwa unaangazia historia mbili, tamaduni mbili, na watu wa nchi hizo mbili ambao wana imani ya kushirikiana, kuheshimiana na kuthaminiana.
Mkurugenzi wa Idara ya Uenezi ya Kamati ya Chama ya Mji wa Chongqing wa China Jiang Hui, ameyaelezea mazungumzo hayo kuwa ni mazungumzo yanayovuka wakati.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma