Rais wa Zanzibar aahidi mustakabali usio na madeni kukiwa na mafanikio makubwa ya maendeleo

(CRI Online) Septemba 03, 2025

Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi amethibitisha tena ahadi ya serikali yake ya kutimiza lengo la kufikia mustakbali usio na deni huku wakiharakisha miradi mikubwa ya maendeleo kote visiwani.

Rais Mwinyi amesema hayo alipotoa hotuba katika Ikulu huko Zanzibar kufuata ziara ya jopo la wanahabari kuhusu mipango inayoendelea ya miundombinu, na kusema serikali ya Zanzibar imeanzisha akaunti maalum ya kulipia madeni ya umma ambapo dola za kimarekani milioni 15 huwekwa kila mwezi, akiahidi kufanya serikali ya Zanzibar iachane na mzigo wa deni.

Rais Mwinyi pia ameeleza kuwa katika awamu yake ya kwanza, serikali yake iliweka kipaumbele maendeleo katika sekta za elimu, afya, miundombinu na upatikanaji wa soko. Hadi sasa barabara za lami zenye urefu zaidi ya kilomita elfu moja zimejengwa huku mapato ya serikali yameongezeka kutokana na kuimarika kwa ukusanyaji wa kodi na kuwezesha huduma ya afya ya umma kuboreshwa zaidi. Sekta nyingine zikiwemo teknolojia ya mawasiliano, uchumi wa buluu na usambazaji wa maji pia zimepata maendeleo makubwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha