Wataalamu wa China wafanya mazungumzo na maofisa wa Sudan Kusini kuhusu usimamizi wa msukosuko

(CRI Online) Septemba 03, 2025

Wataalamu wa China kutoka Chuo cha kimataifa cha mafunzo ya ufundi stadi cha Hunan na maofisa wa Sudan, wameanza semina ya mafunzo kuhusu usimamizi na mwitikio wa msukosuko mjini Juba, Sudan Kusini.

Semina hiyo ya siku 14 iliyofadhiliwa na Wizara ya Biashara ya China inahudhuriwa na watu 30 kutoka Wizara ya masuala ya ubinadamu na Usimamizi wa Majanga ya Sudan Kusini.

Naibu waziri wa masuala ya ubinadamu na usimamizi wa majanga wa Sudan Kusini Bw. Dennis Marial Muorwel Mayom, amesema semina hii inatoa fursa ya kipekee kwa wadau wa kitaifa na kimataifa kubadilishana uzoefu na kujifunza mbinu bora zaidi katika kukabiliana na changamoto.

Ofisa mkuu wa ubalozi wa China nchini Sudan Kusini Huo Ying, amesisitiza haja ya kuimarisha ujenzi wa uwezo kuhusu usimamizi wa msukosuko katika kukabiliana na changamoto za sasa za kimataifa ili kulinda utulivu na maendeleo ya nchi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha