Rais Xi Jinping ahutubia tafrija ya Siku ya Ushindi (V-Day), akisisitiza haki, amani, nguvu ya watu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 04, 2025

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati  Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akihutubia tafrija ya kumbukumbu ya miaka 80 tangu kupatikana ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupambana  na Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti kwenye Jumba la Mikutano ya Umma  la Beijing, Septemba 3, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akihutubia tafrija ya kumbukumbu ya miaka 80 tangu kupatikana ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Septemba 3, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping jana Jumatano wakati akihutubia tafrija ya kumbukumbu ya miaka 80 tangu kupata ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti ametoa wito wa kushikilia kithabiti haki na usawa wa kimataifa, kushikilia kufuata njia ya maendeleo ya amani, na siku zote kufanya juhudi bila kulegalega za kuongeza ustawi wa watu.

Majira ya 5:30 asubuhi, Rais Xi na mkewe Peng Liyuan waliingia kwenye ukumbi wa karamu pamoja na viongozi wa kigeni na wenzi wao walioalikwa kwenye tafrija hiyo.

Rais Xi ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi alisema kuwa ushindi huo unamaanisha mabadiliko ya kihistoria kwa taifa la China -- kutoka kwenye msukosuko katika zama za karibu hadi njia ya ustawishaji mkubwa, na pia hatua kubwa ya mabadiliko katika maendeleo ya dunia.

"Ushindi huu mkubwa ulipatikana kupitia mapambano ya pamoja ya watu wa China pamoja na washirika wa kupinga ufashisti na watu wa duniani kote," Rais Xi amesema.

Amesema, serikali na watu wa China hawatasahau kamwe serikali za nchi mbalimbali na marafiki wa kimataifa ambao waliunga mkono na kusaidia watu wa China katika mapambano yao dhidi ya uvamizi.

Rais Xi akisisitiza kuwa ujenzi wa mambo ya kisasa wa China ni mambo ya kisasa ya maendeleo ya amani, na China daima itakuwa nguvu kwa ajili ya amani, utulivu na maendeleo ya Dunia. "Ni matumaini ya dhati kwamba nchi zote zitajifunza kutoka kwa historia, kuthamini amani, na kufanya juhudi za pamoja ili kusukuma mbele ujenzi wa mambo ya kisasa ya dunia na kujenga pamoja siku nzuri za baadaye za binadamu ," Rais Xi amesema.

Rais Xi Jinping wa China na mkewe Peng Liyuan wakiingia kwenye ukumbi wa karamu pamoja na viongozi wa nchi za nje na wenzi wao  walioalikwa kwenye tafrija ya kumbukumbu ya miaka 80 tangu kupatikana ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan  na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti kwenye Jumba la Mikutano ya Umma  la Beijing, Septemba 3, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais Xi Jinping wa China na mkewe Peng Liyuan wakiingia kwenye ukumbi wa karamu pamoja na viongozi wa nchi za nje na wenzi wao walioalikwa kwenye tafrija ya kumbukumbu ya miaka 80 tangu kupata ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Septemba 3, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati  Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akihutubia tafrija ya kumbukumbu ya miaka 80 tangu kupatikana ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupambana  na Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti kwenye Jumba la Mikutano ya Umma  la Beijing, Septemba 3, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akihutubia tafrija ya kumbukumbu ya miaka 80 tangu kupata ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Septemba 3, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha