

Lugha Nyingine
Rais Xi apongeza ustawishaji wa taifa "usiozuilika" katika kumbukumbu za Siku ya Ushindi
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu kwenye mkutano wa kukumbuka miaka 80 tangu kupatikana ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti mjini Beijing, Septemba 3, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)
BEIJING – Ustawishaji wa taifa la China ni kusikozuilika, amesema Rais wa China Xi Jinping jana Jumatano wakati nchi hiyo ikiadhimisha kumbukumbu ya miaka 80 tangu kupatikana ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupambana dhidi ya Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti.
"Vita hivyo vya mapambano, vikali na vikubwa, vinamaanisha ushindi wa kwanza wa China katika mapambano dhidi ya uvamizi kutoka nje tokea zama za karibu,” amesema Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi, wakati akihutubia mkutano wa kumbukumbu uliofanyika mjini Beijing.
Akisema kuwa ushindi huo ulipatikana chini ya bendera ya umoja wa kitaifa wa kupambana na uvamizi wa Japan ulioanzishwa kwa utetezi wa Chama cha Kikomunisti cha China, alisisitiza watu wa China walitoa mhanga mkubwa katika vita hivyo ambayo ni sehemu muhimu ya Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti, na kutoa mchango mkubwa kwa ajili ya kuokoa ustaarabu wa binadamu na kulinda amani ya dunia.
"Wakati nchi zote duniani zinapotendeana kwa usawa na kwa mapatano, na kuungana mkono ndipo usalama wa pamoja unaweza kulindwa, chanzo kikuu cha vita kuondolewa, na majanga ya kihistoria kuzuiwa," amesema.
Leo, binadamu wanakabiliwa tena na chaguo la amani au vita, mazungumzo au mapambano, na kufanya ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote au kufanya mchezo wa kutiana hasara,” Rais Xi amesema.
Amesema watu wa China watasimama kithabiti kwenye upande sahihi wa historia na upande wa maendeleo ya binadamu, kufuata njia ya maendeleo ya amani, na kuungana na dunia nzima kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
Ametoa wito kwa watu wa makabila yote wa China kuendelea kuwa na mshikamano na kufanya kazi kwa bidii chini ya uongozi imara wa CPC ili kujenga nchi yenye nguvu na kusukuma mbele ustawishaji wa taifa katika sekta zote kwa kupitia ujenzi wa mambo ya kisasa wa China.
Rais Xi ametaka Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) kutoa uungaji mkono wa kimkakati kwa ustawishaji wa taifa na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya amani na maendeleo ya dunia.
Amelitaka jeshi hilo kujijenga kuwa jeshi la kiwango cha juu duniani na kulinda kithabiti mamlaka ya nchi, muungano na ukamilifu wa ardhi ya taifa.
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu kwenye mkutano wa kukumbuka miaka 80 tangu kupata ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti mjini Beijing, Septemba 3, 2025. (Xinhua/Yan Yan)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma