Rais Xi akutana na Rais wa Indonesia Prabowo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 04, 2025

Rais Xi Jinping wa China akikutana na mwenzake wa Indonesia Prabowo Subianto kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Septemba 3, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)

Rais Xi Jinping wa China akikutana na mwenzake wa Indonesia Prabowo Subianto kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Septemba 3, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)

BEIJING - Rais Xi Jinping wa China jana Jumatano alipokutana na mwenzake wa Indonesia Prabowo Subianto, ambaye yuko ziarani nchini China kushiriki kwenye shughuli za maadhimisho ya miaka 80 tangu kupatikana ushindi wa Vita vya Watu wa China dhidi ya Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti amesema kuwa, zikiwa nchi kubwa katika kundi la Nchi za Kusini, China na Indonesia zinapaswa kushirikiana kupinga umwamba wa upande mmoja, kulinda amani na utulivu wa kikanda, na kushikilia haki na usawa wa kimataifa.

Rais Xi amesema kuwa Rais Prabowo amekuja China kushiriki shughuli za maadhimisho hayo licha ya taabu, ikionyesha umuhimu anaoweka kwenye uhusiano kati ya China na Indonesia na urafiki wa dhati wa watu wa Indonesia kwa watu wa China.

"China inaunga mkono utawala wa Rais Prabowo, urejeshaji utaratibu na utulivu wa Indonesia mapema iwezekanavyo, na maendeleo na ukuaji wa Indonesia," Rais Xi amesema.

Rais Xi ameeleza kuwa haijalishi namna gani hali ya kimataifa inavyobadilika, China na Indonesia daima zimekuwa zikisukuma mbele moyo wa uhuru, zikifuata njia ya ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote, na kuonyesha wajibu wa nchi kubwa wa kujiendeleza kwa amani.

"China inapenda kushirikiana na Indonesia kusukuma mbele Kanuni Tano za Kuishi Pamoja kwa Amani na Moyo wa Bandung, na kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya China na Indonesia yenye mustakabali wa pamoja katika ngazi ya juu," Rais Xi amesema.

“Uhusiano na China ni kipaumbele cha juu cha sera ya mambo ya nje ya Indonesia,” Rais Prabowo amesema, akiongeza kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili uko katika kiwango bora zaidi cha historia.

“Indonesia inatazamia kuimarisha ushirikiano na China katika nyanja zikiwemo biashara, uwekezaji, mambo ya fedha na miundombinu,” Rais Prabowo amesema.

Maafisa waadanmizi wa China Cai Qi na Wang Yi walikuwepo kwenye mkutano huo. 

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais Prabowo Subianto wa Indonesia kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Septemba 3, 2025. (Xinhua/Li Xiang)

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais Prabowo Subianto wa Indonesia kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Septemba 3, 2025. (Xinhua/Li Xiang)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha