Lugha Nyingine
Israel yakataa pendekezo la Hamas la kusimamisha vita, yaapa kuendelea na mashambulizi dhidi ya Gaza
Israel imekataa pendekezo la kundi la Hamas la kufikia makubaliano kamili ya kusimamisha mapigano katika Ukanda wa Gaza ikidai jeshi lake litaendelea na mpango wa kufanya shambulizi kubwa dhidi ya mji wa Gaza.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Jumatano, Kundi la Hamas limeeleza tena nia yake ya kutaka kufikia "makubaliano kamili" ambayo yatashuhudia mateka wa Israel wanaoshikiliwa katika Gaza wakiachiliwa huru kwa kubadilishana na idadi iliyokubaliwa ya wafungwa na mahabusu wa Palestina walio katika magereza nchini Israel.
Makubaliano pia yanajumuisha masharti ya kusimamisha mapigano kwa muda mrefu, kuondoka kwa jeshi la Israel kutoka Gaza, kufungua tena vivuko vya mipakani ili kuwezesha usambazaji wa misaada ya kibinadamu na kuanza juhudi za kujenga upya ukanda huo.
Lakini waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametupilia mbali pendekezo hilo na kulielezea kuwa ni la "kupotosha", akisema Israel haitakubali kusimamisha mapigano hadi kundi la Hamas litakapokubali kikamilifu Israel kudhibiti ukanda wa Gaza na kuondolewa nguvu ya kijeshi ya Hamas huko Gaza, kujenga mamlaka isiyo ya kipalestina na kuwaachia huru mateka wote.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



