Kituo cha elimu ya kidijitali kati ya China na Afrika chazinduliwa Tanzania

(CRI Online) Septemba 04, 2025

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam cha Tanzania, kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha ualimu cha Zhejiang cha China, kimezindua Kituo cha Ushirikiano wa Kikanda cha Afrika cha Elimu ya Kidijitali ili kuendeleza muunganisho wa TEHAMA (ICT) katika madarasa ya Afrika.

Hafla ya uzinduzi wa kituo hicho imefanyika katika chuo kikuu hicho, ikiwaleta pamoja maofisa wa serikali, waelimishaji, na wadau wa kimataifa ikisisitiza dhamira ya pamoja ya kuboresha elimu ya kidijitali nchini Tanzania na bara zima la Afrika.

Mkuu wa kitivo cha Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Bw. Nkanileka Mgonda, amesema kituo hicho kitawajengea uwezo walimu kukumbatia uvumbuzi na kuimarisha ushirikiano katika elimu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha