

Lugha Nyingine
Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakutana Tanzania kuhimiza mafungamano na maendeleo
Mkutano wa 58 wa Mawaziri wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) umeanza katika makao makuu yake mjini Arusha, huku Mkutano wa 35 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta Linaloshughulika na Masuala na Mipango ya Jumuiya hiyo ukiendelea.
Taarifa iliyotolewa Jumatano na jumuiya hiyo mikutano hiyo itaendelea hadi Jumamosi, ikiwakutanisha viongozi waandamizi, makatibu wakuu na mawaziri kutoka nchi nane wanachama, ili kujadili masuala ya kimkakati ya sera zinazolenga kuimarisha ushirikiano wa kikanda na maendeleo endelevu.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, mabaraza ya kisekta yanapitia rasimu ya Mkakati wa saba wa Maendeleo ya Jumuiya hiyo, hadidu za rejea za kuhuisha dira ya Jumuiya kuelekea mwaka 2050, na mapendekezo ya sera ya lugha ya eneo hilo.
Aidha, imeeleza kuwa, wajumbe pia wanajadili maendeleo katika kuondoa vizuizi visivyo vya kodi, na shughuli za jumuiya katika nusu ya pili ya mwaka 2025.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma