

Lugha Nyingine
Wanafunzi 50 wa Guinea-Bissau wapokea udhamini wa masomo kutoka kwa ubalozi wa China
(CRI Online) Septemba 04, 2025
Balozi wa China nchini Guinea-Bissau Bw. Yang Renhuo jana Jumatano amewatunuku udhamini wa masomo wanafunzi 50 katika shule ya sekondari ya Kwame N'krumah huko Bissau.
Mkuu wa shule hiyo Bw. Jose Issa Balde, pamoja na wawakilishi wa walimu na wazazi wa wanafunzi walioshinda tuzo walihudhuria hafla hiyo.
Balozi Yang amewapongeza wanafunzi hao, akisema udhamini huo utawasaidia wanafunzi bora wa Guinea-Bissau kukamilisha masomo yao.
Ameeleza matumaini yake kuwa wanafunzi hao watasoma kwa bidii, kujitahidi kupata maendeleo, na kuwa chachu ya maendeleo ya taifa la Guinea-Bissau vilevile kutoa mchango kwa urafiki kati ya China na Guinea-Bissau.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma