

Lugha Nyingine
Banda la China lawa kivutio kwenye maonyesho ya biashara ya filamu barani Afrika
Mkurugenzi Mtendaji Martin Hiller wa FAME Week Africa, ambayo MIP Afrika ni sehemu yake, akizungumza kwenye kipindi cha “Onyesho la China" katika MIP Africa 2025 mjini Cape Town, Afrika Kusini, Septemba 1, 2025. (Xinhua/Wang Lei)
CAPE TOWN - Banda la China limekuwa kivutio kikubwa katika MIP Africa 2025, mojawapo ya shughuli kubwa za kibiashara barani Afrika kwa tasnia ya filamu na televisheni, likiwapa watazamaji wa Afrika lango la kuingia katika sekta ya burudani ya China.
Likiwa limefadhiliwa na Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China na Mamlaka ya Redio na Televisheni ya Taifa ya China, na kuandaliwa na Shirika la Utangazaji la Jiangsu, Banda la China limefuatiliwa wakati wa tukio hilo la Septemba 1-3 likiwa na maudhui mbalimbali ya sauti na video ya Kichina na shughuli nyingi za mawasiliano ya kiutamaduni.
Kivutio kikuu cha Banda la China kilikuwa "Onyesho la China: Kwa Ushirikiano na China" lililofanyika Jumatatu alasiri. Kipindi hicho kiliwasilisha mfululizo wa filamu na televisheni zenye sifa bora za China ambazo zilichanganya mitazamo ya kimataifa na umaalum wa China, kikitoa kwa umma mafanikio ya China katika maendeleo ya filamu na televisheni, na kuimarisha ushirikiano na mawasiliano kati ya taasisi za filamu na televisheni za China na Afrika.
Katika hotuba yake kuu kwenye kipindi hicho cha "Onyesho la China", You Wenze, konsuli mkuu wa China mjini Cape Town, amesema, "China na Afrika zina urithi wa kitamaduni na mvuto wa kipekee, zikiweka msingi wa asili wa sauti kati ya China na Afrika katika uundaji filamu na televisheni. China na Afrika zina makali ya ushindani, na mustakabali wa ushirikiano ni mzuri."
You amesema kuwa mawasiliano na ushirikiano wa kitamaduni kati ya China na Afrika Kusini umeongezeka, akirejelea uzinduzi wa shughuli za "China TV Theatre" wa vituo vya televisheni vya BRICS, ambazo zilianzisha vipindi vya televisheni vya China kwa watazamaji wa Afrika Kusini.
Mkurugenzi Mtendaji Martin Hiller wa FAME Week Afrika, ambayo MIP Afrika ni sehemu yake, amesema kuwa MIP Afrika ilianzishwa ili kuonyesha maudhui ya Afrika kwa watazamaji wa dunia nzima, vilevile kuwezesha uagizaji katika bara. Kwa hiyo, ilikuwa muhimu vile vile kutambulisha maudhui yanayohusiana na watazamaji wa Afrika.
"Huu umekuwa wakati wa kusisimua kwetu sisi MIP Afrika kuikaribisha China kwenye tukio la 2025, na tulifurahi sana kuonyesha miundo mbalimbali, kuanzia tamthiliya na filamu za hali halisi hadi katuni. Inaonyesha tu mvuto wa kimataifa wa maudhui ya Kichina kwa watazamaji wa Afrika," amesema Hiller.
"Kuna fursa nyingi sana za utayarishaji wa pamoja katika sekta ya sauti na video. Ninafurahi sana kuona mijadala mbalimbali katika MIP Afrika ambapo tunaweza kujikita katika maudhui ya Kichina na Kiafrika na kuona jinsi yanavyoingiliana na kuchangamana kati yao," amesema.
Wakati huo huo, katika maadhimisho ya miaka 80 tangu kupatikana ushindi katika Vita vya Watu wa China dhidi ya Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti, Banda la China liliandaa eneo maalum la maonyesho ya mada kwa watazamaji wa kimataifa kutafakari historia na kuthamini amani.
Tukio hilo lilishuhudia usajili wa kampuni zaidi ya 100 za vyombo vya habari, wahudhuriaji zaidi ya 1,500, vilevile ushiriki wa wanunuzi zaidi ya 500 wa kimataifa.
Watu wakitembelea Banda la China katika MIP Africa 2025 mjini Cape Town, Afrika Kusini, Septemba 1, 2025. (Xinhua/Wang Lei)
You Wenze, konsuli mkuu wa China mjini Cape Town, akizungumza kwenye kipindi cha “Onyesho la China" katika MIP Africa 2025 mjini Cape Town, Afrika Kusini, Septemba 1, 2025. (Xinhua/Wang Lei)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma