

Lugha Nyingine
Xi Jinping na Sassou Nguesso watangaza kuinua uhusiano wa pande mbili
Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais wa Jamhuri ya Kongo Denis Sassou Nguesso kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing katika mji wa Beijing, mji mkuu wa China, Septemba 4, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Jamhuri ya Kongo Denis Sassou Nguesso wametangaza jana Alhamisi kwa pamoja kupandisha uhusiano wa pande mbili kuwa jumuiya ya ngazi ya juu yenye mustakabali wa pamoja.
Habari hiyo imetolewa kwenye mkutano kati ya Rais Xi na mwenzake Sassou Nguesso, ambaye alikuwa nchini China kwa kushiriki kwenye shughuli ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 80 tangu kupatikana ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti.
Rais Xi amebainisha kuwa uhusiano kati ya China na Jamhuri ya Kongo unasimama kama mfano wa urafiki kati ya China na Afrika.
"Pande mbili zinapaswa kutumia kikamilifu nguvu bora ya kisiasa ya urafiki na kuaminiana, na kutafuta njia mpya za ushirikiano," Rais Xi amesema.
Katika wakati wa kukabiliwa na dunia yenye mabadiliko na isiyo na utaratibu, China na Afrika, zikiwa wanachama muhimu wa Kusini ya Dunia, lazima zibebe wajibu wa kihistoria wa kuhifadhi haki na usawa wa kimataifa, kulinda amani ya dunia, na kuhimiza maendeleo kwa pamoja.
Kwa upande wake Rais Sassou Nguesso amesema, kupandishwa ngazi kwa uhusiano kati ya China na Jamhuri ya Kongo kumeanzisha mfumokazi mpya kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya pamoja ya nchi hizo mbili.
“Ikiwa mwenyekiti mwenza wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika, Jamhuri ya Kongo inapenda kushirikiana na China kusukuma mbele ushirikiano kati ya China na Afrika na kufikia maendeleo makubwa zaidi” amesema.
Nguesso amesema, “Jamhuri ya Kongo inaunga mkono kikamilifu Pendekezo la Usimamizi wa Dunia lililotolewa na Rais Xi, hili ni pendekezo muhimu ambalo litazinufaisha nchi za Kusini."
Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais wa Jamhuri ya Kongo Denis Sassou Nguesso kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Septemba 4, 2025. (Xinhua/Ding Lin)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma