China na Zimbabwe zapandisha kiwango cha uhusiano kuwa wa jumuiya ya hali zote yenye mustakabali wa pamoja

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 05, 2025

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe, ambaye yuko ziarani nchini China kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 80 tangu  ushindi wa Vita vya Watu wa China dhidi ya Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, mjini Beijing, mji mkuu wa China, Septemba 4, 2025. (Xinhua/Li Xiang)

Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa wametangaza jana Alhamisi mjini Beijing kupandisha kiwango cha uhusiano wa pande mbili kuwa jumuiya ya hali zote yenye mustakabali wa pamoja ambapo tangazo hilo limetolewa kwenye mkutano kati ya Rais Xi na mwenzake Mnangagwa, ambaye alikuwa ziarani nchini China kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 80 tangu ushindi wa Vita vya Watu wa China dhidi ya Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti.

Rais Xi amesisitiza kuwa urafiki unaozidi kuwa wa kina wa "nyota tano" wa nchi hizo mbili umeweka mfano kwa mshikamano na ushirikiano kati ya China na Afrika, na pia kati ya Nchi za Kusini.

"China itaendelea kuiunga mkono bila kuyumba Zimbabwe katika kuchunguza kwa kujitegemea njia ya maendeleo inayolingana na hali yake ya kitaifa na kupinga uingiliaji wa nje na vikwazo haramu," Rais Xi amesema.

Ametoa wito wa kuimarishwa kwa ushirikiano katika ujenzi wa miundombinu, madini, uwekezaji na biashara ili kuimarisha na kuinua uhusiano wa pande mbili.

“China inapenda kushirikiana na Zimbabwe ili kutekeleza matokeo ya Mkutano wa Kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika wa 2024, kutekeleza kwa pamoja Pendekezo la Usimamizi wa Dunia (GGI), kujenga vizuri zaidi Shirika la Kimataifa la Usuluhishi (IOMed), kuimarisha ushirikiano miongoni mwa Nchi za Kusini, na kusukuma mbele maendeleo ya utaratibu wa kimataifa kwa njia ya haki na yenye mantiki zaidi,” Rais Xi amesema.

Kwa upande wake, Rais Mnangagwa ameeleza heshima yake kwa kuhudhuria maadhimisho hayo ya kihistoria nchini China, akisema kwamba jumuiya ya kimataifa inapaswa kukumbuka mchango mkubwa wa China katika ushindi wa Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti, na kushikilia muono sahihi wa kihistoria wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Amesema Zimbabwe inatazamia kuungana na China katika kujenga jumuiya ya hali zote yenye mustakabali wa pamoja, na itaendelea kufuata kanuni ya kuwepo kwa China moja.

Rais Xi Jinping wa China akikutana na mwenzake wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa, ambaye yuko ziarani nchini China kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 80 tangu ushindi wa Vita vya Watu wa China dhidi ya Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, mjini Beijing, mji mkuu wa China, Septemba 4, 2025. (Xinhua/Liu Weibing)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha