Familia ya Jenerali wa Marekani hayati Stilwell yathamini uhusiano wa kudumu na China

(CRI Online) Septemba 05, 2025

Nancy Millward na Susan Cole, ambao ni vitukuu wa Jenerali wa Marekani hayati Joseph Stilwell, ambaye alikuwa kamanda mkuu wa vikosi vya Marekani katika medani ya vita ya China-Burma-India wakati wa kipindi cha Vita vya Pili vya Dunia wameeleza kuthamini kwao uhusiano wa kudumu na China.

Nancy na Susan walialikwa kushiriki kwenye Maadhimisho ya Miaka 80 tangu kupatikana Ushindi wa Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Wajapan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti yaliyofanyika Septemba 3 kwenye Uwanja wa Tian'anmen mjini Beijing, China.

Kabla ya maadhimisho hayo, wanafamilia hao walifunga safari ya kihistoria nchini China, wakisema wanapenda kuendeleza urithi huo wa ushirikiano kati ya China na Marekani wa wakati wa kipindi hicho cha vita.

Hayati Stilwell, alitoa uungaji mkono mkubwa kwa Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Wajapan. Uhusiano huo kati yake na China umerithiwa na familia yake kizazi baada ya kizazi.

Mwaka 1982, mabinti wa Stilwell walianzisha mfuko wa udhamini wa masomo kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wa China kwenda kusoma katika vyuo vikuu vya Marekani. Katika kipindi cha miaka hiyo 40 tangu kuanzishwa kwake, mfuko huo umefadhili makumi ya wanafunzi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha