DRC yatangaza mlipuko wa 16 wa Ebola

(CRI Online) Septemba 05, 2025

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imetangaza kuwa ugonjwa wa Ebola umelipuka katika Jimbo la Kasai, ukiwa ni mlipuko wa 16 tangu mwaka 1976.

Waziri wa Afya wa DRC Bw. Roger Kamba amesema kwenye mkutano na wanahabari kuwa virusi vya aina ya Zaire vya ugonjwa huo vimeibuka tena huko Bulape ambapo watu 28 wanadhaniwa kuambukizwa na miongoni mwao watu 15 wamefariki, wakiwemo wafanyakazi wanne wa afya.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa taarifa ikionya kuwa idadi ya watu walioambukizwa inaweza kuongezeka kutokana na kuenea kwa maambukizi.

Limeeleza kuwa, kwa sasa dozi 2,000 za chanjo ya kujikinga dhidi ya virusi hivyo iliyokuwa ikihifadhiwa mjini Kinshasa itasafirishwa kwenda Kasai, na tani mbili za vifaa kinga na tiba pia zitasambazwa kukidhi mahitaji.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha