

Lugha Nyingine
Jeshi la Uganda laripoti mapambano na kundi la waasi la ADF mashariki mwa DRC
(CRI Online) Septemba 05, 2025
Jeshi la Uganda limesema limepambana na kundi la waasi la Allied Democratic Forces (ADF) siku ya Jumatano kwenye misitu ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo wanajeshi wake wawili wameuawa huku likiwaua wapiganaji watatu wa kundi hilo.
Jeshi la Uganda limetoa taarifa mjini Kampala likisema mapambano hayo yalitokea Apakwang, umbali wa kilomita 40 kaskazini mwa Komanda katika eneo la Mambasa, ambalo liliwahi kuchukuliwa kuwa ngome ya kiongozi wa ADF Musa Baluku.
Limesema kuwa, katika mapigano hayo, bunduki tatu zilipatikana kutoka kwa waasi.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma