Afrika CDC: Idadi ya waliofariki kwa Mpox barani Afrika tangu mwaka 2024 inakaribia 2,000

(CRI Online) Septemba 05, 2025

Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC), kimesema tangu mwanzoni mwa 2024, idadi ya watu waliofariki kutokana na mlipuko wa homa ya Mpox barani Afrika inakaribia 2,000, huku idadi ya watu wanaoambukizwa homa hiyo ikiendelea kupungua.

Akiongea kwa njia ya mtandao kwenye mkutano na wanahabari, naibu meneja wa Afrika CDC anayeshughulikia matukio ya Mpox Bw. Yap Boum II, amesema tangu mwanzoni mwa kwa mwaka jana nchi 29 za Afrika zilizoathiriwa zimeripoti maambukizi 185,994, ambapo miongoni mwa maambukizi hayo, 51,969 yalithibitishwa, na vifo 1,987 vilirekodiwa.

Takwimu kutoka kwa wakala maalum wa huduma ya afya wa Umoja wa Afrika zinaonyesha kuwa hadi kufikia mwaka huu, bara la Afrika limeripoti jumla ya maambukizi 105,697, na kupita jumla ya mwaka jana ya 80,297.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha