Utalii wa kiikolojia wachochea uchumi wa wenyeji wa Mji Xiongjiang, Mkoani Fujian, China (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 08, 2025
Utalii wa kiikolojia wachochea uchumi wa wenyeji wa Mji Xiongjiang, Mkoani Fujian, China
Picha iliyopigwa Septemba 6, 2025 ikionyesha mandhari nzuri ya bustani katika Mji Xiongjiang wa Wilaya ya Minqing, Mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China. (Xinhua/Zhou Yi)

Katika miaka ya hivi karibuni, Mji Xiongjiang wa Wilaya ya Minqing, Mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China umekuwa ukihamasisha wenyeji kukarabati nyumba za vijijini na kutumia maeneo yasiyotumika kwa kuendeleza shughuli za utalii kwenye mazingira ya kiikolojia, ambapo watalii wanaweza kujionea kilimo cha sifa maalumu, kukaa kwenye hoteli za kiraia na kutembelea vijiji vyenye mandhari nzuri. Jitihada hiyo imevutia vijana kadhaa wajasiriamali kuanzisha biashara.

Kwa sasa, mji Xiongjiang kila siku kwa wastani unapokea watalii zaidi ya 1,700, na idadi ya watalii wanaweza kufikia 18,700 kwa siku wakati wa wikendi na likizo.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha