Mwalimu wa kijijini alinda usafiri wa watoto wa kuvuka mkoa kwenda shuleni kwenye mpaka wa mikoa ya Hunan na Guizhou, China (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 11, 2025
Mwalimu wa kijijini alinda usafiri wa watoto wa kuvuka mkoa kwenda shuleni kwenye mpaka wa mikoa ya Hunan na Guizhou, China
Picha ya droni ikionyesha Ren Dabing na wanafunzi wake wakivuka mto wakati wakiwa njiani kurudi nyumbani baada ya masomo katika Kijiji cha Wansen cha mji Yajia wa Wilaya inayojiendesha ya Kabila la Wamiao ya Songtao, Mkoa wa Guizhou, kusini-magharibi mwa China, Septemba 9, 2025. (Xinhua/Yang Wenbin)

Shule ya Msingi ya Molao Youyi iko katika Kijiji cha Molao cha Mkoa wa Hunan, katikati mwa China, ambayo inazungukwa na Mto Huayuan unaopakana na Kijiji cha Wansen katika Mkoa wa Guizhou kusini magharibi mwa China, na imeanzishwa na kusimamiwa kwa pamoja na serikali za mikoa ya Hunan na Guizhou. Wanafunzi kutoka Kijiji cha Wansen upande wa Guizhou wanapaswa kupanda feri ili kuvuka Mto Huayuan kwa ajili ya kwenda shule.

Ren Dabing, mwalimu kutoka Kijiji cha Wansen, kwa sasa ni mwalimu pekee mzaliwa wa Guizhou katika Shule hiyo ya Msingi ya Molao Youyi.

Tangu mwaka 2006, Ren amekuwa akibeba kwa hiari jukumu la kuwasindikiza wanafunzi kuvuka mto huo kwenda na kurudi shuleni. Feri hiyo, ambayo awali ilikuwa ni mashua ndogo ya mbao, imefanyiwa maboresho kadhaa na kwa sasa ni feri ya kisasa cha boti.

Katika miaka 19 iliyopita, mwalimu Ren amekuwa akilinda kwa kuwajibika usafiri wa watoto wa kuvuka mkoa kwenda shuleni kwenye mpaka wa mikoa wa Hunan na Guizhou bila ripoti za matukio yanayohusika na usalama.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha