Mwandishi wa habari ashuhudia urafiki kati ya China na Guinea ya Ikweta katika shule iliyojengwa kwa msaada nchini China (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 12, 2025
Mwandishi wa habari ashuhudia urafiki kati ya China na Guinea ya Ikweta katika shule iliyojengwa kwa msaada nchini China
Milagrosa Ada Micha Abeso, mwandishi wa habari wa Guinea ya Ikweta, akicheza na watoto wa Shule ya Msingi ya Urafiki kati ya China-Guinea ya Ikweta katika Wilaya inayojiendesha ya makabila ya Wamiao, Wayao na Wadai ya Jinping ya Mkoa wa Yunnan, Kusini-magharibi mwa China, Septemba 9, 2025. (Xinhua/Peng Yikai)

Tangu zianzishe uhusiano wa kidiplomasia zaidi ya nusu karne iliyopita, China na Guinea ya Ikweta zimekuwa zikisaidiana katika dhiki na faraja na kudumisha ushirikiano wa kivitendo na mawasiliano katika sekta mbalimbali, vikileta matokeo halisi.

Mwezi Aprili 2015, Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, Rais wa Jamhuri ya Guinea ya Ikweta, alitangaza kwamba nchi yake itatoa msaada wa kujenga shule katika Wilaya inayojiendesha ya Makabila ya Wamiao, Wayao na Wadai ya Jinping ya Mkoa wa Yunnan, Kusini-magharibi mwa China. Ujenzi wa Shule ya Msingi ya Urafiki kati ya China na Guinea ya Ikweta ulikamilika mwaka uliofuata, na tangu wakati huo shule hiyo imesimama kama ushuhuda wa urafiki wa kudumu wa nchi hizo mbili.

Mei 27, 2024, Rais Obiang alizungumza kwa njia ya video na wanafunzi wa shule hiyo wakati wa ziara yake nchini China. Watoto waliimba shairi la enzi ya Tang na nyimbo za makabila yao.

Kwa sasa, wanafunzi zaidi ya 2,000 kutoka makabila 16 wanapata masomo yao katika shule hiyo ya msingi, ambapo alama za urafiki kati ya China na Guinea ya Ikweta ziko kila mahali. Mapambo yake yanaangazia jiografia, desturi na bidhaa za Guinea ya Ikweta, huku chumba cha maonyesho kikionyesha sanaa zilizotengenezwa na wanafunzi kwa kusherehekea urafiki kati ya nchi hizo mbili. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha