Mbinu za kijadi za kutengeneza mkate wa naan zarithiwa na kuendelezwa Xinjiang, China (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 12, 2025
Mbinu za kijadi za kutengeneza mkate wa naan zarithiwa na kuendelezwa Xinjiang, China
Rishit Himit akifungasha mikate ya naan mjini Kuqa, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini-magharibi mwa China, Julai 22, 2025. (Xinhua/Wang Jingqiang)

Kuna msemo katika Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini-magharibi mwa China kwamba mtu anaweza kukaa bila nyama kwa siku tatu, lakini si kwa siku moja bila mkate wa naan. Unadhihirisha nafasi isiyo na mbadala ya mkate huo wa naan katika maisha ya kila siku ya watu wa makabila yote mkoani humo. Miongoni mwa aina zaidi ya 200 za mkate huo wa naan zinazopatikana Xinjiang, mkate wa naan wa Kuqa unachukuliwa kuwa "mfalme" ukiwa na kipenyo cha wastani wa zaidi ya nusu mita.

Uokaji mkate huo wa naan wa Kuqa ni wenye uhitaji mwingi zaidi wa kitaalamu kuliko kuoka aina nyingine za mkate huo wa naan.

Unga wa ngano huwa wenye kunyumbulika baada ya kukandwa mara kwa mara. Kinyunya hutandazwa na chombo chenye sindano hutumiwa kutengeneza miundo ya mduara. Viungo maalum hupakwa sawasawa, ikifuatiwa na kunyunyizia mbegu za sesame. Wakati tanuri la shimo likibanika na mkate huo wa naan ukiwa umebandikwa kwenye upande wa ndani, harufu ya ngano iliyookwa hupanda mara moja.

Rishit Himit, mwenye umri wa miaka 65, ni mrithi mwakilishi wa ngazi ya kitaifa wa urithi wa utamaduni usioshikika wa mbinu za kijadi za kutengeneza mkate huo wa naan. Kila asubuhi kabla ya mwanga wa jua kuamsha mitaa ya Kuqa, harufu nzuri ya ngano ya mikate hiyo ya naan kwenye duka lake huanza kujaza hewa.

Rishit alianza kujifunza ujuzi wa kutengeneza mikate ya naan kutoka kwa baba yake akiwa na umri wa miaka 18, na sasa amerithisha ufundi huu wa kipekee kwa wanawe. Kila siku, wakaazi wenyeji na watalii humiminika kwenye duka lake la mikate ya naan. Kufikia mwisho wa siku, mikate mikubwa ya naan elfu moja au mbili iliyotengenezwa na Rishit, wanawe na wanafunzi wake yote inakuwa imeuzwa.

Mkoani Xinjiang, mkate wa naan si tu chakula cha kutosheleza njaa bali pia ni kiungo kinachounganisha maisha ya kila siku na urithi wa kitamaduni. Kuanzia maduka ya mikate ya naan katika mitaa ya zamani ya Kuqa hadi ukumbi wa maonyesho ya mambo ya mkate wa naan katika Gulio Kubwa la Urumqi, mkate huo wa naan unakumbana na umma kwa uwepo dhahiri zaidi.

Mkate wa Naan huja katika maumbo na ladha mbalimbali zinazovutia, zikiufanya kuwa zawadi ya lazima kununuliwa na watalii.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha