Ghana na China zapanua ushirikiano zikilenga biashara na uwekezaji

(CRI Online) Septemba 16, 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ghana Samuel Okudzeto Ablakwa amesema, Ghana na China zinapanua kidhahiri uhusiano wa pande mbili kupitia uhusiano wenye nguvu wa kidiplomasia, ushirikiano wa kina wa kiuchumi, na mapendekezo ya pamoja ya maendeleo.

Akizungumza jana katika kikao cha kazi za Wizara hiyo katika miezi minane iliyopita, Ablakwa amesema Ghana ni kati ya nchi za mwanzo za Afrika kufaidika na ushuru sifuri wa China kwa bidhaa zinazotoka katika nchi za Afrika. Pia amesema wameanza majadiliano kuhusu mapendekezo kadhaa, ikiwemo kuanzishwa kwa viwanda vya kuunganisha magari ya umeme, na kuanzishwa kwa safari za moja kwa moja za ndege kati ya miji mikubwa ya Ghana na ile ya China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha